https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

WENYEJI, Arsenal usiku wa jana wameibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Aston Villa katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Emirates Jijini London.
Mabao ya kikosi cha kocha Mikel Arteta yalifungwa na Thomas Partey dakika ya 23, Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 46 na ushei na Emile Smith Rowe dakika ya 56, kabla ya Jacob Ramsey kuifungia Aston Villa la kufutia machozi dakika ya 82.
Arsenal inafikisha pointi 14 baada ya ushindi huo na kusogea nafasi ya tisa, wakati Aston Villa inabaki na pointi zake 10 katika nafasi ya 13 kufuatia wote kucheza mechi tisa.