BABA WA ALISSON BECKER AFARIKI DUNIA AKIOGELEA BWAWANI BRAZIL

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Alisson Becker (lkushoto) akiwa na baba yake, Jose (kulia) amefariki dunia baada ya kuzama kwenye bwawa ziwani nchini Brazil 

BABA wa makipa Alisson wa Liverpool na Muriel wa Fluminense, Jose Agostinho Becker amekutwa amekufa akiwa ana umri wa miaka 57.
Alikuwa anaogelea jirani na nyumbani kwake kwenye bwawa huko Lavras do Sul, kilomita 320 kutoka Porto Alegre, kusini mwa Brazil kabla ya maji kumshinda na kuzama kisha kupotea tangu Jumatano.
Iliripotiwa amepotea tangu Jumatano Saa 11 jioni kwa saa za huko kabla ya mwili wake kupatikana Saa 7:50 Alhamisi usiku.
Jose Agostinho Becker naye pia alikuwa kipa wa timu ya ridhaa ya ndiye alichangiua mno hata wanaye, Alisson na Muriel kuwa makipa bora.

Previous Entries WAHAMIAJI HARAMU 83 PAMOJA NA WASINDIKIZAJI WAWILI WAFUNGWA JELA MKOANI PWANI Next Entries Waziri Jafo ataka Zimamoto, Skauti wakomeshe majanga ya moto shuleni.