Beki wa Madrid Sergio Ramos kuikosa Liverpool tena, akutwa na Corona

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Nahodha wa timu ya taifa ya Hispania na klabu ya Real Madrid Sergio Ramos amekutwa na maambukizi ya Virusi vya Corona. Kwa sasa Ramos yupo nje ya uwanja kutokana na majeraha ya misuli.

Ramos amekuwa nje ya uwanja tangu Aprili 1, 2021, kutokana na majeruhi ambayo yamemfanya akose michezo ya hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Liverpool, lakini pia aliukosa mchezo mkubwa dhidi ya mahasimu wao FC Barcelona siku ya Jumamosi mchezo amabao Real Madrid ilishinda kwa mabao 2-1.

Kwa mujibu wa taarifa za kitabibu mlinzi huyo anatarajiwa kurejea tena uwanjani mwishoni mwa mwezi huu. Hivyo kukutwa na maambukizi ya Covid-19 hukuta hadhiri sana kurejea kwake uwanjani, isipo kuwa kwa sasa hataruhusiwa kufika katika viunga vya mazoezi vya Real Madrid mpaka pale atakapo pimwa tena na kukutwa hana maambukizi.

Ramos mwenye umri wa miaka 35 amekuwa akisumbuliwa na majeruhi msimu huu, mwezi Februari alifanyiwa upasuaji wa goti kabla ya kuumia tena.

Mchezaji huyo mwandamizi ndani ya Los Blancos ameshaichezea klabu hiyo jumla ya michezo 670 na amefunga mabao 101 tangu alipojiunga na miamba hiyo ya ulaya mwaka 2005 akitokea Sevilla

The post Beki wa Madrid Sergio Ramos kuikosa Liverpool tena, akutwa na Corona appeared first on Bongo5.com.

Previous Entries Majaliwa: Serikali Imetumia Sh. Bilioni166.17 Kugharimia Elimumsingi Next Entries CWT YAWEKA MSIMAMO WA KUPINGA UANZISHWAJI WA BODI YA KITAALUMA YA WALIMU [TANZANIA TEACHERS PROFESSIONAL BOARD.]