https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainabu Chaula ( kushoto ) akikabidhi tuzo ya  Taasisi bora ya Fedha kwenye matumizi ya Tehama kwa Ofisa Mkuu Mwendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (katikati) pamoja na Ofisa Mkuu wa Tehama wa Absa, Emmanuel Mwinuka, wakati wa Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), jijini Arusha jana.

 Ofisa Mkuu Mwendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (kushoto)  na Ofisa Mkuu wa Tehama wa Absa, Emmanuel Mwinuka, wakionyesha tuzo ya Taasisi Bora ya Fedha  kwenye matumizi ya Tehama mara baada ya kukabidhiwa wakati wa Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), uliofanyika jijini Arusha jana

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk. Zainabu Chaula (kulia), akibadilishana mawazo na Ofisa Mkuu Mwendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (wa pili kushoto) pamoja na Ofisa Mkuu wa Tehama wa Absa, Emmanuel Mwinuka (kushoto),  wakati wa Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), uliofanyika jijini Arusha jana. Mwingine ni mmoja wa waandaaji wa mkutano, Tumaini Magila.