https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi (wa pili kushoto), akimkabidhi cheti cha shukrani Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Letshego, Simon Jengo (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Andrew Tarimo (wa pili kulia) kwa udhamini wa Kongamano la Biashara na Uchumi lililofanyika jijini Dodoma, jana. Wengine ni Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Mayoda Economic Development Group, Sophia Simbu (kushoto) na Mwenyekiti Mtendaji wa Mayoda, Agustino Matefu.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Letshego, Andrew Tarimo akisisitiza jambo wakati akiwasilisha mada wakati wa Kongamano la Biashara na Uchumi lililofanyika jijini Dodoma, jana. Kongamano hilo liliandaliwa na Taasisi ya Mayoda Economic Development Group kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Meneja wa Uendelezaji Biashara Benki ya Letshego, Ruth Mpangalala (kushoto) akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Vijana na Ajira, Patrobas Katambi (kulia) mara baada ya kufungua Kongamano la Biashara na Uchumi lililofanyika jijini Dodoma, jana. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Andrew Tarimo.