Bilionea namba moja Afrika Aliko Dangote hajakata tamaa kuinunua Arsenal (+ Video)

Bilionea wa Nigeria Aliko Dangote, ambaye ndiye mtu tajiri zaidi Afrika kwa mara nyengine amehusishwa na jaribio la kuinunua Arsenal , kitu ambacho amekuwa akijaribu kufanya tangu 2011.


Kuhusishwa kwake na mabingwa hao wa mara 14 wa kombe la FA kunajiri kufuatia ripoti kwamba kamapuni kubwa ya kusafisha gesi na mafuta anayomiliki kandokando ya mji wa Lagos inadaiwa kwamba inakaribia kukamilika mapema 2021. Amekuwa akitumai kwamba itampatia pato la kuweza kuinunua klabu hiyo ya mjini London .

Dangote amenukuliwa akisema kwamba ataanza harakati za kuinunua klabu hiyo baada ya kukamilisha kampuni hiyo ya mafuta.{90min}

Bofya hapa chini kutazama.

https://www.instagram.com/p/CLv6NtQhlbC/

The post Bilionea namba moja Afrika Aliko Dangote hajakata tamaa kuinunua Arsenal (+ Video) appeared first on Bongo5.com.

Previous Entries Sekta Ya Hifadhi Ya Jamii Kuchochea Kasi Ya Maendeleo Ya Kiuchumi Nchini Next Entries VIDEO Mary Boyoi ft Harmonize – All I Need