Bobi Wine Afanya Tamasha la Kwanza Tangu Ashtakiwe

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Nyota wa muziki wa pop na mbunge wa upinzani nchini Uganda ‘Bobi Wine’ amefanya tamasha lake kwanza tangu ashtakiwe na kufungwa kwa mshtaka ya uhaini.

Katika tamasha hilo la Bobi Wine kulikuwa na idadi kubwa ya polisi, ambapo liliruhusiwa tu kufanyika kwa sababu halikuwa la kisiasa.

Aidha, Bobi Wine anadaiwa kuteswa na kupigwa akiwa kizuizini mwezi Agosti mwaka huu, madai ambayo yalikanushwa na mamlaka.

Umaarufu wake miongoni mwa vijana nchini Uganda unaonekana kuwa changamoto kubwa kwa rais wa nchi hiyo Yoweri Museveni.

Baadhi ya maelfu ya watu waliohudhuria katika tamasha hilo walikuwa wamevalia nguo nyekundu, rangi inayohusishwa na vuguvugu la Bobi Wine la People Power.

Watoto wa Uganda waonesha jumba walilonunuliwa na French Montana
“Ninashukuru polisi wa Uganda kwa kutupa ulinzi mkubwa kwa ajili ya usalama wetu, lakini sio kama hapo awali walipokuwa wakituzuia,”amesema Bobi Wine

Previous Entries MANJI ASIPORUDI JANUARI 15, MWAKANI MKUCHIKA ATAWAAMBIA NINI WANA YANGA? Next Entries Agoma Kutoka Jela, Adai Anafundisha Wafungwa Kutumia Facebook