Bodi ya Mikopo yapokea maombi 74,000, yaongeza siku tano

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza siku tano za wanafunzi kuendelea kuomba mkopo kwa njia ya mtandao hadi Agosti 23, lengo likiwa ni kutoa fursa kwa waombaji ambao hawajakamilisha maombi yao.

Taarifa ya HESLB kwa umma iliyotolewa
na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru, ilisema kuwa walianza
kupokea maombi ya mikopo Julai Mosi, mwaka huu na mwisho ilikuwa iwe
jana.

Alisema Badru katika taarifa
yake kuwa HESLB imepokea maombi kutoka kwa baadhi ya waombaji mikopo ambao
hawajakamilisha maombi yao kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kukosa nyaraka
muhimu.

 “Ingawa hadi leo (jana) tumeshapokea
maombi zaidi ya 74,821 yaliyokamilika kwa njia ya mtandao, tumepokea pia
maombi kutoka kwa wateja wetu wakitaka kuongezewa muda ili wakamilishe nyaraka
muhimu kama nakala za vyeti vya vifo vya wazazi wao, barua kutoka kwa wadhamini
wao na nyaraka nyinginezo, tumewasikiliza na kuongeza muda,” alisema Badru.

 Aliwataka
waombaji mikopo ambao hawajakamilisha maombi yao, kutumia muda ulioongezwa
kukamilisha maombi yao kwa kuwa hawataongeza muda zaidi baada ya Agosti 23.

 “Tunasihi waombaji wetu watumie muda huu
ulioongezwa kukamilisha maombi yao kwa kuwa hatutaongeza tena.

“Baada ya Agosti 23 tutaanza
kufanya uchambuzi wa maombi tuliyopokea ili tuwapangie mikopo wenye sifa kwa
wakati na tupeleke fedha za mikopo vyuoni kabla vyuo havijafunguliwa,” alisema
Badru.

Katika kipindi kilichoongezwa
cha hadi Agosti 23, Badru alisema dawati la huduma kwa wateja la HESLB litakuwa
wazi ili kutoa ufafanuzi kwa waombaji mkopo pale utakapohitajika.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5
Previous Entries Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa hii, Pogba mipango ya kuonda United ipo pale pale, Sanchez na wengine sokoni Next Entries Mjumbe wa NEC atolewa povu kumlazimisha askari kusalimia kwa salamu ya CCM