CANAF 2021 UPDATES- Uganda v/s Sierra Leon

Na. John Mapepele

Kipindi cha kwanza kimemalizika huku Timu ya Siera Leon inaongoza kwa mabao mawili dhidi ya Uganda katika mchezo wa mashindano ya Afrika ya soka kwa wenye ulemavu CANAF 2021 unaoendelea katika hivi sasa kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mchezo huu umetawaliwa na mvua kubwa hata hivyo timu zote zinapambana kiume hadi kumaliza kipindi cha kwanza.

Bao la kwanza limefungwa katika dakika ya 15 na goli la pili limefungwa dakika ya  18 ya kipindi cha kwanza.

Mvua kubwa iliyonyesha imesababisha kushindwa kuendelea na mchezo kutokana na maji kujaa katika uwanja.

Jitihada zinaendelea za kutoa  maji ili kuendelea na mchezo.

Mchezo huu wa leo asubuhi, Novemba 28, 2021 ni wa pili ambapo mchezo wa kwanza wa ufunguzi katika mashindano haya umechezwa jana na Timu ya Tanzania  kuibuka mshindi dhidi Morocco kwa magoli 2-1.

Mchezo huu umechezeshwa na Refa Devid Mang’ong’o , Agnes Alphonce toka Tanzania na  Muhamed Mwadin toka Zanzibar

Mchezo unaofuata leo asubuhi hii ni dhidi ya mabingwa watetezi wa  Angola na Zanzibar na utachezwa Hassan Magega Haji Omary na Catherine Thobias

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5