Dola Bilioni Moja za Changwa Kwaajili ya Ujenzi wa Kanisa la Notre Dame

Kiasi cha fedha dola bilioni moja kimechangishwa kutoka kwa waumini wa kawaida na watu wenye uwezo na umaarufu kutoka duniani kote kwa ajili ya ujenzi mpya wa kanisa kuu la kihistoria la Notre Dame mjini Paris nchini Ufaransa baada ya kuharibiwa vibaya na moto.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameongeza shinikizo kwa kutangaza muda wa miaka 5 wa kukarabatiwa upya kanisa hilo la karne ya 12.

Leo Rais Macron anaendesha kikao maalum cha baraza la mawaziri kitakachojikita katika suala la tukio la moto la Notre Dame.

Mjumbe anayehusika na turathi na utamaduni Stephane Bern ameliambia shirika la habari la kifaransa la France Info leo kwamba dola milioni 995 zimeshachangishwa mpaka sasa ambapo wachangiaji ni watu maarufu wakiwemo wamiliki wa makampuni makubwa ya urembo ya L’Oreal, Chanel na Dior. Maafisa wanalichukulia tukio hilo la moto kama ajali.

Previous Entries ATCL kuanza safari za kwenda Afrika Kusini Next Entries Mke wa Kisena kuunganishwa na mumewe kesi ya uhujumu uchumi