Dreamliner Boeing 787 yaanza Safari za nje yapeleka Mbuzi Dubai

Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, amethibitisha kuwa ndege ya shirika la ndege Tanzania ATCL Boeing 787 Dreamliner, imebeba shehena ya nyama ya Mbuzi kutoka Mwanza kuipeleka moja kwa moja Dubai.

Akiongea leo jijini Mwanza, wakati wa kupakia nyama hiyo Mongela amesema safari hiyo ina tija kwa watazanzia kutokana na bidhaa bora ambayo itakuwa inafika sokoni kwa wakati.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

”Serikali imefanikiwa kusafirisha mzigo wa kwanza wa nyama, kimsingi mzigo unaopakiwa leo hapa Mwanza unafika Dubai leoleo na hii ni biashara ya kimataifa ambayo unahitaji kufikisha bidhaa bora sokoni”, amesema Mongela.


Naye Mkurugenzi wa kampuni inayosafirisha nyama hiyo, amesema hiyo ni fursa kwa wafugaji wadogo kwani biashara hiyo ikifanikiwa itasaidia kupanua soko hivyo bei ya mifugo hiyo itapanda na kuwanufaisha wafugaji.

Safari hiyo ni ya kwanza ambapo zitafanyika safari zingine mbili na kama zitakuwa na mafanikio itaanzishwa safari ya kila siku kwa ajili ya kupeleka mzigo mkubwa zaidi.

Previous Entries Jose Mourinho akataa dili nono la kuinoa klabu hii kubwa barani Ulaya Next Entries URUSI: Wanasayansi Waliogundua Bomu Linaloenda Kwa Kasi zaidi Duniani Wakamatwa, Watuhumiwa Kwa Uhaini