Fei Toto: Tutashinda leo mechi yetu na Kengold ya Mbeya

FEISAL Salum, kiungo wa Klabu ya Yanga amesema kuwa wana amini kwamba watapata ushindi kwenye mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora dhidi ya Kengold ya Mbeya.

Uwanja wa Uhuru saa 10:00 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa ambapo timu ambayo itashindwa kupata matokeo itatolewa jumlajumla.

Feisal amesema kwa namna ambavyo wamejiandaa inawapa nafasi kupata ushindi ndani ya uwanja kwenye mchezo huo muhimu.

“Tupo sawa na tunaamini kwamba kila mchezaji anahitaji kuona timu ikishinda hivyo tutapambana kupata matokeo ndani ya uwanja.

“Inawezekana kupata ushindi na nafasi yetu ipo pia tunawaheshimu wapinzani wetu hilo lipo wazi kwa kuwa nao pia wanahitaji ushindi,” .

Previous Entries Wananchi Wa Lushoto Waishukuru Serikali Kuwarejesha Shughuli Za Uzalishaji Katika Kiwanda Cha Kuchakata Chai Cha Mponde Next Entries Saudia yakanusha Bin Salman kuhusika na kifo cha Khashoggi