Leo muhula mpya wa masomo kwa mwaka 2019 umeanza. Taasisi yetu ambayo ni walezi wa Shule ya Msingi Msinune tunaendelea na utaratibu wetu wa kugawa vifaa vya kujifunzia kwa wanafunzi na vifaa vya kufundishia kwa walimu vitakavyotumika kwa mwaka mzima.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Kwa mwaka 2019, watoto 284 wa Shule ya Msingi Msinune kila mmoja kapata begi la shule, kalamu za wino 50 , kalamu za risasi 50 na vifutio ambavyo vitakidhi mahitaji yao kielimu kwa mwaka huku wazazi wakitimiza mahitaji mengine yaliyobaki. Upande wa walimu taasisi imetoa kalamu, chaki, rejista za masomo na karatasi (reams) kwa ajili ya kudurufu (copy) mitihani na kazi za masomo.

Tukiongelea mafanikio ya Taasisi shuleni Msinune, mpaka mwaka jana tumefanikiwa kukamilisha ujenzi na ukarabati wa madarasa, ofisi za walimu, vyoo kwa ajili ya walimu na wanafunzi na mradi wa maji safi.

Kwa mwaka 2019-21 Tutajikita zaidi kwenye ujenzi wa nyumba za walimu shuleni kutatua changamoto ya makazi ya walimu shuleni hapo kwa kushirikiana na wadau mbali mbali . Mafanikio ya hili yatajenga mazingira rafiki zaidi kwa walimu kufanya kazi na kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Bado tunazidi kuwaasa Watanzania kuendelea kujitolea kwa namna moja au nyingine katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa elimu bora nchini.

2019,FLAVIANA MATATA FOUNDATION ,MSINUNE PRIMARY SCHOOL