FRESH JUMBE AWAOMBA BASATA KUENZI MCHANGO WA MARIJAN RAJAB

*Akoshwa na Diamond na alikiba

Na.Khadija seif,Globu ya jamii.


NGULI wa muziki dansi barani la Afrika kutoka nchini Tanzania fresh jumbe awatia hamasa kubwa wajapani kujifunza kiswahili kupitia muziki wake.

Jumbe amezungumza na michuzi tv na kuweka wazi kuwa kwa kiasi kikubwa sana wajapani wameweza kujua kiswahili kutokana na muziki ambao amekuwa akifanya kwa muda mrefu sana na kupendwa na watu wengi.

“Wajapani,wachina na watu wengine kutoka mataifa mbalimbali wamekua wakivutiwa sana na muziki wangu kupelekea kutamani kujua kilichoimbwa kuanzia kufahamu matamshi mpaka maneno yaliyoimbwa katika wimbo huo,”

Aidha ,jumbe amesema soko la muziki wa Tanzania limepiga hatua kwa kiasi kikubwa sana na kupelekea vijana wengi kuiepeperusha bendera kwa kupitia sanaa mbalimbali hususani muziki.

“Katika nchi ambazo utazitaja basi huwezi kuacha kuitaja Tanzania kuwepo kwa wanamuziki wanaopendwa sana hivyo tunajitoa kifua mbele ukilinganisha na hapo zamani ni wachache ambao tulikua tunafahamika tena kwa nchi chache lakini kwa sasa hakuna nchi ambayo muziki wa bongofleva haujapata kupenya,”

Amewataja Diamond platinum,Alikiba ndio wasanii ambao anavutiwa na kazi zao kutokana na ubunifu wa hali ya juu wakati wa upishi wa nyimbo zao na kuweka vionjo ambavyo vimewazolea mashabiki wengi ndani na nje ya nchi.

Aidha , ameweka bayana sababu zinazopelekea baadhi ya nyimbo zake kuendelea kupendwa ni kutokana na mashairi ambayo yanaishi na kusadifu maisha halisi wimbo kama penzi ni kikohozi,pamela ,conjesta pamoja na mazingira yetu .

Pia ameomba Baraza la sanaa (BASATA) pamoja na wanamuziki wote nchini kuenzi juhudi za marehemu Marijan Rajab kwa kuweka picha au ukumbusho ambao vizazi vijavo vitaweza kutambua mchango wake kupitia muziki wake.

“Bila jitihada zake na uwezo wa kutambua kipaji changu nisingewezakufika huku nilipo na mbali na hilo marijan amewezakutambulisha vizuri nchi ya Tanzania kwa kupitia miondoko ya muziki wa dansi kwa vionjo vya kiafrika zaidi na ustadi mzuri wa kukuza lugha ya kiswahili kwa vibao vyake kama “masudi,mtaa wa Saba,ndoa ya mateso, mwanameka ,namsaka mbaya wangu na vibao vingine vingi”,

Kwa sasa fresh jumbe amesema anaendelea na harakati za muziki wa dansi sanjari na kuwa mtayarishaji wa muziki.
.. mwisho