Hizi Hapa Sababu za Kagame Kumsamehe Mpinzani Wake

Hizi Hapa Sababu za Kagame Kumsamehe Mpinzani Wake

Ilhali kukiwa na muendelezo wa matukio ya kuachiwa kwa viongozi wa upinzani nchini Rwanda, imeelezwa kuwa nchi hiyo imelazimika kufanya hivyo kwa ajili ya kupata uwanja mpana zaidi wa kuandaa mkutano wa 26 wa nchi za jumuiya za madola mwaka 2020 (Commonwealth Heads of Goverment 2020).

Jana kupitia Mahakama Kuu mjini Kigali, ilimuachia huru aliyekuwa mpinzani wa Rais wa Paul Kagame kwenye uchaguzi wa mwaka 2017, Diane Rwigara  pamoja na Mama yake ambaye walishtakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo ukwepaji kodi.

Sambamba na kuachiwa huru kwa kiongozi huyo, mwezi septemba 2018 Mahakama nchini humo iliamuru kuachiliwa huru kwa zaidi ya watuhumiwa 2000 wa kisiasa nchini Rwanda akiwemo aliyekuwa mpinzani wa Rais Kagame kwenye uchaguzi wa Urais wa mwaka 2010, Victoire Ingabire jambo ambalo lilianza kutiliwa shaka kwenye medani za siasa barani afrika.

Imeelezwa huenda serikali nchini humo imelazimika kufanya hivyo kutokana na matakwa ya nchi za Jumuiya ya Madola kupitia mkutano wake wa 25 ambao ulifanyika Uingereza ambapo uliridhia maombi ya Rwanda kuandaa mkutano baada ya kushindikana kufanyika nchini Malaysia kutokana na hali ya kisiasa.

Rwanda imelazimika kufanya hivyo kwaajili ya kukwepa adhabu ya kufungiwa kuwa mwanachama wa Jumuiya hiyo kwa kuwa moja ya sehemu ya vigezo vya umoja huo kwa wanachama wake ni kutimiza masharti ya kuwa na demokrasia bora kwenye nchi zao.

Mbali na kukwepa adhabu hiyo pia Rwanda imelenga namna ambavyo nchi hiyo itanufaika kupitia ugeni huo, ambao takribani mataifa 53 yanatarajiwa kuhudhuria ambayo yatasaidia kuongeza uchumi wa nchi hiyo.

Mkutano huo unaojulikana kwa jina la CHOGM 2020, utakuwa wa kwanza kufanyika kwa nchi ambazo hazijawahi kuwa koloni la Uingereza ambapo pamoja na mambo mengine, hujadili juu ya fursa za uchumi, demokrasia na masuala ya utamaduni.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5