JKT QUEENS HAWANA CHA MSALIA MTUME, LEO WAISHUSHIA MVUA YA MABAO YANGA PRINCESS


KIKOSI cha Yanga Princess leo kimepoteza kwa kuchapwa mabao 8-1 dhidi ya JKT Queens kwenye mchezo wa Ligi ya Wanawake Tanzania maarufu kama Serengeti Lite Women’s Premier League.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

JKT Queens wanafanikiwa kuwafunga watani wote wa jadi baada ya kuanza na Simba Uwanja wa Karume kwa kuifunga bao 1-0 na leo wameendeleza ubabe wao kwa Yanga Princess kwa ushindi wa mabao 8-1.

Yanga Princess wanafanikiwa kuifunga JKT Queens kwani mpaka sasa baada ya kucheza michezo sita walikuwa hawajafungwa bao hata moja.

Alliance Girl wameshinda bao 6-0 dhidi ya Evergreen Queens, Baobab Queens wameshinda mabao 3-1 dhidi ya Mapinduzi Queens. 
Previous Entries LEOPARDS WALIVYOJIFUA LEO DAR KUJIANDAA NA KOMBE LA SPORTPESA Next Entries YANGA SC ILIYOTEMBEZA UBABE KAMPALA 1993 HAUTASAHAULIKA