https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

BAO pekee la mshambuliaji Dickson Mhilu dakika ya 39 limewapa wenyeji Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar jioni ya leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba mkoani Kagera.
Ushindi huo wa kwanza katika michezo minne ya mwanzo, kufuatia kufungwa 1-0 na Yanga nyumbani na sare mbili mfululizo, 1-1 na Namungo mjini Lindi na 0-0 na 0-0 naq Mbeya City hapo hapo Kaitaba unaifanya Kagera Sugar ya kocha Mkenya, Francis Barasa ifikishe pointi tano.
Hali ni mbaya kwa Mtibwa Sugar ya kocha Mcameroon, Joseph Omog ikifikisha mechi nne bila ushindi, kufuatia kufungwa 1-0 na Mbeya Kwanza Mlandizi na sare mbili 0-0 Tanzania Prisons Dar es Salaam na 1-1 na Geita Gold huko Geita.