Kala Jeremiah , Rayvanny, Zuchu, Mbosso jukwaa moja, Rais Samia akizungumza na vijana wa Mwanza (Video)

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Kala Jeremiah, Peter Msechu, Mbosso, Zuchu,B endi ya muziki wa dansi T.O.T na wengine wengi wamekonga nyoyo za Wanamwanza walipotumbuiza katika mkutano wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alipokua akizungumza na Vijana katika viwanja vya nyamagana leo juni 15,2021.

Mashabiki na viongozi mbali mbali wameonekana wakisimama kila wasanii hao walipopanda jukwaani kutoa burudani lakini hasa alipopanda msanii wa kike kutoka lebo ya WCB Zuchu ,ambae alionekana kupokelewa kwa shangwe nyingi na Wanamwanza ambao walikua wakiimba nae pamoja nyimbo zote alizokua akiimba.

BY – BAKARI WAZIRI

The post Kala Jeremiah , Rayvanny, Zuchu, Mbosso jukwaa moja, Rais Samia akizungumza na vijana wa Mwanza (Video) appeared first on Bongo5.com.

Previous Entries SERIKALI KUKAMILISHA UJENZI WA KITUO KIKUBWA CHA UKUZAJI VIUMBE MAJI IFIKAPO SEPTEMBA MWAKA HUU Next Entries Tanzania inakadiriwa kuwa na kiwango kikubwa cha ndoa za utotoni duniani -Rebeca