KAMPUNI ya Uzalishaji na Usindikaji wa kahawa Amimza ya mkoani Kagera imelipongeza Shirika la Viwango Tanzania(TBS) kwa kazi kubwa wanayoifanya na hasa kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa na zile zinazoingizwa nchini zinakuwa kwenye ubora wa hali ya juu.

Akizungumza katika hafla fupi ya utoaji cheti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa nchini iliyofanyika Makao makuu ya TBS ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, Mkurungezi Mtendaji wa Amimza, Amir Hamza amesema kwa sasa kampuni hiyo inayonafasi kubwa ya kupeleka  kahawa nje ya nchi  kutokana na kukidhi Kwa ubora uliothibitishwa na Shirika hilo.

Akizungumza zaidi zao hilo la kahawa amesema  awali walikuwa wakikumbana na chagamoto pindi wanapopeleka kahawa katika masoko ya nje kutokana na kutokuwa na cheti cha mfumo wa usalama wa chakula lakini hivi sasa wanaamini wanakwenda kufanya vizuri zaidi.

“Cheti hiki cha alama  za ubora na mfumo wa usalama wa chakula ni kitu ambacho kinatakiwa katika ulimwengu wa sasa hasa pale unapopeleka bidhaa katika mataifa ya nakwamba tunamshukuru kwa hatua hii kubwa ambayo awali ilikuwa ni historia kwetu,”amesema

Amesema  wanywaji wengi wa kahawa ya Amimza walikuwa walikuwa wakidai vyeti vya uthibitisho wa ubora na usalama wa chakula hivyo kupata cheti hicho ni fahari kwa kiwanda hicho na taifa kwa ujumla kwani.kunakuwa na uhakika wa bidhaa inayodhalishwa.

“Kwa sasa kahawa ya Amimza itakuwa inafanana na kahawa za nje ya nchi zenye ubora zaidi kwa ajili ya matumizi ya binadamu hivyo watanzania nao wajizoweshe kunywa kahawa .”amesema

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Na kuongeza kuwa “Tunatarajia kuona masoko yakifunguka zaidi na Uzalishaji kuongezeka zaidi na huko nyuma tulikuwa tukipeleka katika nchi 7 tu za ulaya ambao kwa sasa soko litaongezeka zaidi.”

Hamza amesema Bara la Afrika linakunywa kahawa zaidi ya asilimia 20 ya kahawa yote inayozalishwa duniani hivyo Kampuni Amimza itapata nafasi kubwa ya kupeleka kahawa kutokana na kuwa na cheti cha alama za ubora kilichothibitishwa na Shirika la viwango nchini.

Hata hivyo amesema kwa sasa masoko yatapanuka zaidi nakwamba hata  wakulima wataifaidika sana  kupitia zao hilo.

Ameongeza  Kampuni hiyo kufanya kazi ikiwa na  mashine ndogo ya kukoboa kahawa lakini hadi kufikia sasa amefanikiwa kujenga kiwanda kikubwa sana nakuwa mfano bora  barani Afrika.

Hamza amesema Kampuni hiyo imefanikiwa kutoa ajira mbalimbali kwa watanzania na lengo kuu nikuona kampuni yake inatoa ajira nyingi zaidi hususani Kwa vijana.

Aidha  ajenda ya  Serikali ya awamu ya tano na sita ya Tanzania ya Viwanda imesaidia kwa kiasi kikubwa  kwa wazalishaji wa bidhaa kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye ubora.