Lingard ageuka lulu

Klabu za Paris St-Germain, Real Madrid na Inter Milan zinamfuatilia winga Jesse Lingard kabla ya dirisha la usajili halijafunguliwa mwishoni mwa msimu.

Lingard, 28, anang’ara kwa sasa ambapo anachezea klabu ya West Ham kwa mkopo akitokea Manchester United.

Ripoti zinadai kuwa Arsenal wapo katika rada pia ya kusaka saini ya nyota huyo wakati ambapo kocha Mikel Arteta akionekana kama kuwa ndiyo chaguo namba moja.

The Gunners watakutana na kizuizi kikubwa kutoka kwa West Ham kutokana na mchezaji huyo kuwa katika wakati mzuri kwa sasa akiwa tayari ameshafunga jumla ya magoli nane (8) katika Premier League tangu atuwe kwa mkopo akitokea Manchester United.

Ingawaje hakuna kipengele cha kumnunua moja kwa moja katika makubaliano ya mkopo wa pauni milioni tatu, lakini Lingard atakuwa nje ya mkataba Old Trafford mwishoni mwa msimu ujao na hivyo maisha yake ya baadae yanategemea na dirisha hili la usajili.

The post Lingard ageuka lulu

appeared first on Bongo5.com.
Previous Entries Tarime: Watu watatu wafariki kufuatia kubomoka kwa daraja Next Entries WAKAAZI WA BINGUNI WAOMBA KUSHIRIKISHWA KATIKA UJENZI WA HOSPITALI KATIKA WILAYA HIYO