Lissu Atilia Mkazo Nia Yake ya Kugombea urais 2020

Mwanasiasa na mwanasheria wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema), Tundu Lissu, ametilia mkazo nia yake ya kugombea urais 2020, endapo atapata wito kutoka kwa wananchi na chama chake kugombea nafasi hiyo.

Lissu ametoa msisitizo huo alipozungumza na chombo cha habari cha VoA, alipokuwa nchini Marekani na kueleza kipaombele chake endapo atapata nafasi hiyo.

” Nimeshatangaza utayari wangu wa kugombea nafasi hiyo nikiteuliwa na chama changu na ninarudia tena nikipata wito wa kugombea urais nitapokea wito huo.” amesema Lissu

Lissu ambaye yupo nje ya nchi tangu mwezi Septemba 7, mwaka juzi kwaajili ya matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi ameshikilia msimamo wake huo wa kugombea urais licha ya hivi karibuni kubainisha kuwa hatarejea nchini hadi hapo chama chake kitakapo mhakikishia usalama wake.

Wanafunzi watano wafa maji Morogoro
Ametaja malengo yake iwapo atafanikiwa kuteuliwa na chama chake kugombea urais, amesema atarejea upya mchakato wa kutengeneza katiba mpya ya wananchi ili kuwapatia wananchi katiba bora.

Lissu amekuwa Mbunge kwa vipindi viwili, alivuliwa ubunge wake mwaka huu kutokana na sabau ambazo spika wa bunge, Job Ndugai alizitoa za utoro bungeni na pia kutokujaza fomu za maadili ya watumishi wa umma ambazo hutakiwa kujazwa pia na wabunge wote.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5
Previous Entries NEC: Watanzania wengi wamepoteza kitambulisho cha mpiga kura Next Entries Simba, Yanga Kibaruani Leo