Mabosi Yanga Wajifungia Kumhoji Metacha Mnata

HATMA ya kipa wa Yanga, Metacha Mnata, inatarajiwa kujulikana leo mara baada ya Kamati ya Nidhamu ya timu hiyo kukutana kusikiliza utetezi wake.
 
Kipa huyo, hivi karibuni alisimamishwa na uongozi wa Yanga baada ya kufanya utovu wa nidhamu dhidi ya mashabiki timu hiyo kufuatia mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting takriban wiki tatu zilizopita, Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam. Yanga ilishinda 3-2.
 
Akizungumza na Championi Ijumaa,Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga Haji Mfikirwa alisema kuwa kamati hiyo itakutana kwa ajili ya kusikiliza utetezi wake kabla ya maamuzi mengine kutolewa kwa uongozi.“Hatima ya Metacha itajulikana kesho (jana).
 
Hilo suala hivi sasa lipo kwenye Kamati ya Nidhamu iliyopo ndani ya Yanga na halipo kwa viongozi, hivyo baada ya kamati hiyo kukutana tutapewa viongozi na kutoa taarifa.
 
“Ninaamini hilo suala litafikia muafaka mzuri na hatima ya kipa huyo itajulikana baada ya kikao hicho cha Kamati ya Nidhamu kukutana na Metacha,” alisema Mfikirwa.
Previous Entries MSHAMBULIAJI WA POLISI TANZANIA AVUNJIKA MIGUU YOTE MIWILI BAADA YA TIMU KUPATA AJALI LEO ASUBUHI IKITOKEA MAZOEZINI MOSHI Next Entries Oxfam: Idadi ya watu wanaokufa njaa inapita ile ya vifo vya covid