Na Said Mwishehe,Michuzi TV

PAMOJA na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha katika Jiji la Dar es Salaaam zaidi ya saa sita maelfu ya wananchi wa majimbo ya Ubungo na Kibamba wamejitokeza katika mkutano wa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli.

Maelfu hayo ya wananchi wa majimbo ya Ubungo na Kibamba katika Wilaya ya Ubungo wamejitokeza katika mkutano wa kampeni wa Dk.Magufuli uliofanyika Uwanja wa Barafu uliopo kata ya Mburahati jijini.

Hata hivyo tangu mapema asubuhi , jijini Dar es Salaam lilikuwa na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo mbalimbali lakini mvua hiyo haikuwa sababu ya kuwafanya wananchi wasijitokeze katika mkutano huo.

Pamoja na mvua hiyo maelfu ya wananchi kwa upendo wao mkubwa na mahaba waliyonayo kwa Dk.Magufuli walifika katika mkutano mapema kabisa.Dk.Magufuli alifika katika mkutano huo saa nne asubuhi lakini maelfu ya wananchi hao walifika tangu saa 12 asubuhi wakiwa na furaha na shauku ya kumuona na kumsikiliza.

Akizungumza mbele ya maelfu ya wananchi hao Dk.Magufuli amewaambia kwamba wananchi hao wamemuonesha upendo mkubwa sana kwani pamoja na mvua kubwa illnayonyesha bado wamemsubiri kumsikiliza.

“Wananchi wamekubali  kunyeshewa mvua kwasababu ya upendo wao mkubwa wangu.Upendo huu nitalipa mara 100, ni upendo mkubwa sana.Nimezunguka katika maeneo mengi lakini naomba niseme kutoka moyoni mmenionyesha upendo mkubwa ambao sijawahi kuona,sikutarajia.

“Upendo ambao mmenionyesha hili ni deni kubwa kwetu, najua nitashinda urais katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu,najua wagombea ubunge na wagombea madiwani mtawaleta tutawalipa kwa kufanya kazi ya kuleta maendeleo makubwa,”amesema Dk.Magufuli.

Amewahakikishia wananchi hao kuwa kwa upendo ambao wamemuonesha leo hii hatawaacha, atakuwa nao bega kwa bega katika kuleta maendeleo ya wananchi.

Wakati akiendelea kuzungumza na wananchi hao Dk.Magufuli amesema mvua hiyo na matone ambayo yamewadondokea katika mkutano huo iwe baraka na neema ya kuleta mabadiliko ya wananchi.”Mateso ya leo ambayo mmeyapata kwa kunyeshewa na mvuu hii ikawe baraka kwa wananchi wote .

“Heshima ambayo mmenipa leo sitausahau, upendo ambao mmenipa leo nitauweka rohoni mwangu,upendo ambao nimeupata ni wa hali ya juu sana, niwaahidi nitawalipa maendeleo,”amesema Dk.Magufuli na kusisitiza upendo alioneshwa ataulipa kwa kuwaletea maendeleo.
 
Pamoja na mambo mengine Dk.Magufuli amewaambia wananchi hao kwamba anafahamu kuna maendeleo makubwa ambayo yamefanyika bado atafanya makubwa zaidi kwani anatambua kuna changamoto ya miundombinu ya barabara za lami, lakini kwa upendo ambao wameunesha atahakikisha anaweka lami katika barabara za mitaani ambazo zitapendekezwa na wabunge na madiwani wa CCM ambao watachaguliwa Oktoba 28 mwaka huu.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Mgombea UIrais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia maelfu ya wananchi wa majimbo ya Kibamba na Ubungo Uwanja wa Barafu wa Mburahati katika mkutano wake wa tatu wa kampeni mkoani Dar es salaam leo Jumanne Oktoba 13, 2020