Mahakamani yatoakauli Wema Sepetu apelekwa India kutibiwa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imesema itatoa amri endapo msanii wa filamu nchini Wema Sepetu atashindwa kuwasilisha uthibitisho wa nyaraka za matibabu yake.

Hatua hiyo imetokana na mshtakiwa huyo kutofika mahakamani hapo kwa mara mbili mfululizo kwa madai kuwa ni mgonjwa na yupo nchini India kwa ajili ya matibabu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 13 mwaka huu na mahakama imesema endapo Wema hataleta vielelezo hivyo, mahakama itatoa amri.

Amri hiyo imetolewa leo, Mei 29, 2018 na Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Thomas Simba, baada ya mdhamini wa Wema, Mariam Sepetu ambaye ni mama yake mzazi kuwasilisha mahakamani tiketi ya ndege badala ya nyaraka za matibabu.

Wema kutumia siku mbili kuishawishi mahakama isimuadhibu Wakili wa Serikali Costatine Kalula, ameieleza mahakama kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya washtakiwa hao kujitetea, lakini mshtakiwa wa kwanza Wema hakuwepo Mahakamani.

Baada ya Kakula kueleza hayo mahakamani, Mariam Sepetu alisimama na kuieleza mahakama kuwa, Wema ni mgonjwa tangu  Mei 14, mwaka huu na sasa yupo India kwa ajili ya matibabu.

“Mheshimiwa hakimu, Wema yupo nchini India kwa ajili ya matibabu, ameenda kufanyiwa upasuaji kwa sababu tangu siku ile. (Mei 14, 2018) hali yake si nzuri na hapa tuna fomu ya matibabu, tunaomba kuzitoa mahakamani,” amedai mama yake.

Baada ya kuwasilisha fomu hizo za matibabu na kupitiwa na Wakili wa Serikali zilibainika kuwa si fomu za matibabu badala yake zilikuwa nyaraka za tiketi ya ndege.

The post Mahakamani yatoakauli Wema Sepetu apelekwa India kutibiwa appeared first on Zanzibar24.

Previous Entries VIJANA 966 WAHITIMU MAFUNZO YA KIJESHI MLALE JKT Next Entries EXIM BANK YAFUTURISHA WATEJA WAKE MWANZA