https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Msanii wa BongoFleva Barakah The Prince, amesema kuna watu wanaishi kwenye mahusiano bila ya kuwa na Ndoa za halali na hata yeye anamchukulia mpenzi wake Najma, kama Mke wake japokuwa hajamuoa.

Barakah The Prince ameeleza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuulizwa kwanini huwa anamuita Najma mke wake bila hata kuwa na kibali cha Ndoa.

“Sijasema kama ni Mke wangu ila ninavyomchukulia ni kama Mke, kwanza sio kila mtu anayeishi na mwanamke ni mke wake kwa sababu watu wengi wanaishi kwenye ndoa ambazo si za halali na hawajafunga ndoa, lakini ukiishi naye mwanamke ndani na unamuita Mke wako” amesema Barakah ThePrince.

Aidha msanii huyo ameongeza kuwa “Kwa mimi ninavyomchukulia Najma ni kama Mke wangu, na yeye anavyonichukulia ni kama Mume wake na sijasema kama ni Mke wangu au mimi ni mwanaume wake”.

Barakah pia amesema kuwa mawasiliano ya mara kwa mara ndiyo yanafanya yeye na Najma kuwa pamoja japokuwa mpenzi wake huyo yuko mbali.