Mama Kanumba Acharuka Baada ya Kusikia Lulu Michael Anaolewa

WAKATI maandalizi ya harusi ya mwigizaji Elizabeth Michael ‘Lulu’ yakiwa yamepamba moto chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda, mama mzazi wa aliyekuwa mwigizaji maarufu wa Bongo Movies, marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amecharukia tukio hilo.

Mama Kanumba amefunguka kuwa, endapo atapelekewa kadi ya mwualiko wa harusi hiyo hawezi kwenda kwa sababu tangu atoke gerezani hawajawahi kuonana wala kusalimiana naye.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Mama Kanumba aliliambia Ijumaa Wikienda kuwa, hata hiyo habari yenyewe ya Lulu kuolewa na Francis Shiza ‘Majizo’ anaisikia kwenye vyombo vya habari na kwamba hajui lolote.

Alisema kuwa, anajua wazi kwamba si rahisi kwa wahusika kumpelekea mualiko huo nyumbani kwake.

“Kwanza hiyo habari yenyewe nimeisikia kwenye vyombo vya habari, lakini mimi sijui kabisa kama wanaweza kuniletea hiyo kadi ya mwaliko na hata wakiniletea siendi.

“Najua itakuwa ngumu tu katika mazingira tuliyopitia sisi, kwanza mimi sasa hivi muda mwingi ninajikalia nyumbani tu kutoka na maradhi yangu haya presha,” alisema Mama Kanumba.

Hivi karibuni, Makonda alitangaza kuwa mwenyekiti wa shughuli hiyo ya harusi ya Lulu inayotajwa kuwa itakuwa ya kihistoria mara tu baada ya staa huyo kumaliza kifungo chake cha nje anachokitumikia kwa sasa baada kukutwa na hatia ya kumuua bila kukusudia Kanumba ambaye alikuwa mwandani wake.

Stori: Imelda Mtema, Dar

Previous Entries NGOMA AWASILI SALAMA AFRIKA KUSINI, KUFANYIWA VIPIMO LEO Next Entries Public Notice : Higher Education Students' Loans Board (HESLB)