MAMIA WAJITOKEZA MAZISHI YA DADA WA MBUNGE WA JIMBO LA SINGIDA MAGHARIBI

Waombolezaji wakishusha kaburini jeneza lenye mwili wa Lucylight Ndekeja ambaye ni dada yake Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu wakati wa mazishi yake yaliyofanyika katika makaburi ya Kanisa la Katoliki Parokia ya Sepuka wilayani Ikungi mkoani Singida jana.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya mazishi nyumbani kwao na marehemu Kata ya Sepuka.
Baadhi ya wafanyakazi wenzake na marehemu na waombolezaji wengine wakiwa kwenye ibada hiyo.
Waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya mazishi nyumbani kwao na marehemu Kata ya Sepuka.
Ndugu jamaa na marafiki wakiwa kwenye ibada hiyo. Wa tatu kutoka kulia ni mume wa marehemu.
Mjomba wa marehemu akiwa ameshika tama kwenye ibada hiyo.
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida, Elekizandya Katabi (kushoto) na Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Novatus Kibaji wakiomba kabla ya kushiriki sakramenti takatifu katika ibada hiyo.
Mbunge Mteule wa Jimbo la Singida Mashariki, Miraji Mtaturu akitoa salamu za rambirambi katika ibada hiyo.
Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Ikungi, Mika Likapakapa alitoa salamu za rambirambi.Wengine ni viongozi kutoka kata zote za jimbo hilo wakisubiri kutoa rambirambi zao.
Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, Elekizandya Katabi akikabidhi rambirambi kwa mmoja wa wanafamilia ya Marehemu.
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Kingu akitoa shukurani kwa niaba ya wanafamilia kabla ya kufanyika mazishi hayo.
Mazishi yakifanyika
Padre wa Kanisa Katoliki Parokia ya Yoseph Mfanyakazi ya Mandewa, Paterine Mangi, akisimika msalaba juu ya kaburi la marehemu Lucylight Ndekeja baada ya kukamilika kwa mazishi.
Mama wa marehemu akiweka shada la maua kwenye kaburi la mtoto wake.
Mume wa marehemu akiwa shada la maua kwenye kaburi na mke wake.
Watoto wa marehemu wakiweka shada la maua kwenye kaburi la mama yao. 
Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi na Singida Mashariki, Elibariki Kingu na Miraji Mtaturu (kulia) wakiweka kaburini shada la maua.
Previous Entries MAJALIWA AZUNGUMZA NA WACHEZAJI TIMU YA SOKA YA NAMUNGO NA KUWAKABIDHI MIPIRA Next Entries AUDIO | Beka Ibrozama - Mahabuba | Download