MAN UNITED YAICHAPA TOTTENHAM HOTSPUR 3-1 LONDON

TIMU ya Manchester United leo imewachapa wenyeji, Tottenham Hotspur mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Tottenham Hotspur Jijini.
Mabao ya Manchester United yamefungwa na Fred dakika ya 57, Edinson Cavani dakika ya 79 na Mason Greenwood dakika ya 90, wakati la Spurs limefungwa na  Son Heung-Min dakika ya 40.
Kwa ushindi huo, Manchester United imefikisha pointi 63 baada ya kucheza mechi 31, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi 11 na vinara, Manchester City ambao hata hivyo wamecheza mechi moja zaidi.

Previous Entries VIDEO Agness Suleiman – WANIPA Next Entries VIDEO Anjella ft Harmonize – Kama