TIMU ya Manchester United imezidi kujiondoa kwenye mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya England baada ya kulazimishwa sare ya 3-3 na Everton jana Uwanja wa Old Trafford – na sasa inazidiwa pointi mbili na vinara, Manchester City (47-45) ambao pia wana mechi mbili mkononi.
Mabao ya United yalifungwa na Edinson Cavani dakika ya 24, Bruno Fernandes dakika ya 45 na Scott McTominay dakika ya 70, wakati ya Everton yamefungwa na Abdoulaye Doucoure dakika ya 49, James Rodríguez dakika ya 52 na Dominic Calvert-Lewin dakika ya 90 na ushei