https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa KMC ni timu makini hivyo amewataka wachezaji kucheza kwa tahadhari kesho katika Uwanja wa Taifa.

Yanga itavaana na KMC kesho ikiwa ni mchezo wake wa nane wa Ligi Kuu Bara, imefanikiwa kushinda mechi sita na kupata sare mchezo mmoja na kufikisha jumla ya pointi 19.

“Mechi yetu na KMC itakuwa ngumu kutokana na jinsi vijana wa timu hii wanavyojitolea uwanjani, ni wachezaji wazuri nimewasoma na kujua jinsi wanavyocheza.

“Nawatambua vizuri wapinzani, tumefanikiwa kuboresha kikosi tofauti na tulivyocheza na Alliance kwani tulicheza vibaya, hivyo nimetumia nafasi hiyo kuboresha makosa yaliyojitokeza tusiyarudie,”alisema.