Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam nchini Tanzania imewafutia dhamana, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mbunge wa Tarime Mjini (CHADEMA), Esther Matiko baada ya wawili hao kukiuka masharti ya dhamana.

Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo leo Novemba 23, Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema watuhumiwa hao wawili wameshindwa kuzingatia masharti ya dhamana katika kesi ya uchochezi inayowakabili.

Wakili wa upande wa utetezi, Peter Kibatala amesema kuwa wata kata rufaa kupinga uamuzi huo wa mahakama.

Kutokana na uamuzi huu wa Mahakama, Mbowe na Matiko watapelekwa rumande wakati taratibu za kukata rufaa zikiendelea