Mkopo wa Tsh. Milioni 194 watolewa kwa wanawake, vijana na walemavu wilayani Njombe

Jumla ya vikundi 86 vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu halmashauri ya wilaya ya Njombe vimepatiwa mikopo yenye thamani ya Tsh. Milioni 194 kwa mwaka wa fedha 2018/2019.

Mikopo hiyo iliyotolewa kwa awamu mbili,awamu ya kwanza halmashauri hiyo ilitoa mikopo ya thamani ya Tsh. Milioni 66 mnamo february 2019 katika vikundi 36 huku awamu ya pili ikitolewa Tsh Milioni 128 katika vikundi 50.

Katika kipindi hicho cha 2018/2019 vikundi vya wanawake vimeonekana kuongoza kupatiwa mikopo kwa kuwa na vikundi 59,vijana 22,watu wenye ulemavu Vikundi vitano.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Njombe Bi. Ruth Msafiri  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika makabidhiano ya mikopo hiyo amewataka wanufaika wa mikopo hiyo kuitumia ipasavyo katika kujikwamua kiuchumi pamoja na kuirejesha kwa wakati ili Serikali kupitia halmashauri ya Njombe iendelee kutoa mikopo mingine kwa wahitaji

The post Mkopo wa Tsh. Milioni 194 watolewa kwa wanawake, vijana na walemavu wilayani Njombe appeared first on Zanzibar24.

Previous Entries Download Audio: Jopa The Don – Inogeshe Next Entries Trump akatisha mahojiano kisa msaidizi wake kakohoa