MKUDE, CHAMA WAMTISHA IBENGE

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

 

KOCHA Mkuu wa AS Vita ya DR Congo, Florent Ibenge amesema kuwa anaamini kama wachezaji  Clatous Chama na Jonas Mkude watacheza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi yao siku ya Ijumaa basi watapata wakati mgumu katika mchezo huo.

Mara ya mwisho kwa Simba na AS Vita kukutana, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1, huku bao la ushindi la Simba likifungwa na Clatous Chama katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar.

Mkude pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba ambacho kilicheza na Vita katika mechi ya kwanza nchini Congo ambapo Simba walipoteza kwa mabao 5-0.

Akizungumzia maandalizi yao kuelekea mchezo huo, Ibenge amesema “Nawakumbuka wachezaji wengi wazuri ndani ya kikosi cha Simba kama Clatous Chama na Jonas Mkude, kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi yao ambao tulipoteza, nakumbuka Chama ndiye alitufunga bao lililotutoa kwenye mashindano.“

“Lakini pia namkumbuka Mkude alicheza vizuri, nadhani wachezaji hao wanahitaji ulinzi zaidi ili wasitupe madhara kuelekea mchezo huu ambao tutakuwa nyumbani.“

 

 

Previous Entries EX wa Boateng afariki Dunia wiki moja baada ya kuachana Next Entries MREMBO AGANDISHA NYWELE ZAKE KWA GUNDI KIMAKOSA....HALI NI TETE, SASA ATAKA AOMBEWE TU