MOROCCO YAAGA AFCON U20, NI UGANDA NA TUNISIA NUSU FAINALI

TIMU ya Morocco imtupwa nje ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 (AFCON U20) baada ya kufungwa kwa penalti 4-1 na Tunisia kufuatia sare ya 0-0 jana Uwanja wa Olimpiki de Nouakchott Jijini Nouakchott.
Nayo Gambia ilikamilisha idadi ya timu za Nusu Fainali baada ya ushindi wa 3-0 dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), mabao ya Wally Fofana dakika ya tano,  Momodou Bojang dakika ya 49 na Alieu Barry dakika ya 90 na ushei.
Mechi za Nusu Fainali zitachezwa Jumatatu, Ghana na Gambia na Uganda na Tunisia hapo hapo Uwanja wa Olimpiki wa Nouakchott.
Ghana iliitoa Cameroon kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 1-1 na Uganda iliita Burkina Faso kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5
Previous Entries SIMBA SC 3-0 AFRICAN LYON (KOMBE LA TFF) Next Entries GAMBO AAHIDI KUFUATILIA UTATUZI WA CHANGAMOTO YA BARABARA YA BARACUDA-SORENYI KATA YA BARAA