MRADI WA KUJENGEA UWEZO WATAALAM NA WAKULIMA KATIKA KILIMO CHA AUMWAGILIAJI WAFANIKIWA KWA KIASI KIKUBWA. DODOMA


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Marco Ndonde akifungua mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji. Uliyofanyika Jijini Dodoma.
Bw. Ukombeso Emmanuel Afisa Kilimo kutoka Manyara akiongea na waandishi wa Habari hawapo katika Picha kuhusu faida iliyopatikana kutokana na mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji, katika Mkutano wa wadau uliofanyika Jijini Dodoma leo.
Katika Picha ni sehemu ya Washiriki katika majadiliano ya kubadilishana mawazo kuhusu mradi wa mafunzo na matunzo wa skimu za kilimo cha Umwagiliaji. Iliyofanyika Jijini Dodoma.

Imeelezwa kuwa , Mradi wa kujengea uwezo kwa wakulima na wataalamu katika Kilimo cha Umwagiliaji nchini umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia matumizi ya muongozo yakinifu wa umwagiliaji na Mafunzo ya uendeshaji na matunzo ya skimu za umwagiliaji katika maeneo ya mfano yaliyo chaguliwa na mradi huo.

Hayo yamelezwa Leo Jijini Dodoma na kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Marco Ndonde alipofungua warsha ya wadau na wataalam ya kubadilishana malengo na mbinu zitakazotumiwa kufanya mafanikio ya mradi kuwa endelevu ili kuwezesha ukuzaji wa sekta ya umwagiliaji kote nchini. .

Bw. Ndonde amesema kuwa, mradi huo umekuwa wa mafanikio kwa kiasi kikubwa kutokana na wadau wa kilimo hicho kutumia mwongozo wa umwagiliaji kwa umakini katika kutekeleza shughuli zote za kilimo cha Umwagiliaji.

Akiongea katika Warsha hiyo, Afisa Kilimo kutoka Ofisi za Kilimo cha umwagiliaji Manyara Bw. Lukombeso Emmanuel, amesema Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika eneo la umwagiliaji kupitia Mradi huo jambo ambalo limewawezesha wakulima wenyewe kuweza kupata uelewa hususan katika eneo la matunzo ya miundombinu ya umwagiliaji jambo ambalo awali muamko ulikuwa mdogo.

“Kwa upande wetu sisi kama wataalam katika ngazi zote tumejengewa uwezo juu ya uibuaji, , utekekelezaji, uendeshaji na mafunzo pamoja na ufuatiliaji na tathmin kwa kufuata mwongozoyakinifu wa Umwagiliaji na namna ya kuwawezesha wakulima kufanya shughuli zao kufuata Mwongozo huo.” Alisisitiza Bwana Lukumbeso

Pamoja na mafanikio hayo mradi umekuwa na changamoto mbalimbali kwa wakulima kama vile uelewa mdogo kuhusu Sheria, kanuni na Miongozo ya Kilimo cha Umwagiliaji jambo ambalo linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kupitia kuitambulisha rasmi Sheria ya Umwagiliaji kwa wadau mbalimbali na kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.

Awamu hiyo ya pili ya mradi wa kujengea uwezo wakulima katika Kilimo cha Umwagiliaji unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa kushirikiana na Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5
Previous Entries Statement ya Simba SC Kuhusu Kauli ya Kabwili wa Yanga SC Next Entries Kumbe Stamina Ndiyo Alianza Kusaliti Tangu zamani