MSHAMBULIAJI Gerald Mathias Mdamu amevunjika miguu yote miwili baada ya kikosi cha Polisi Tanzania kupata ajali leo asubuhi kikitokea mazoezini Uwanja wa Chuo cha Polisi (TPC), Moshi mkoani Kilimanjaro.
Afisa Habari Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya Saa 5:00 asubuhi wakati timu ikitoka mazoezini kwenye uwanja wa TPC uliopo kwenye Kiwanda cha sukari na kusababisha wachezaji 16 kuumia na kulazwa hospitali ya KCMC.
Pamoja na Mdamu aliyeumia zaidi na kuvunjika miguu yote miwili, wengine ni Abdullazizi Mkame, Pius Buswita, Daruweshi Saliboko, Deusdedity Cossmas, Salum Ally, Abdulmalik Adam, Idd Mobby, Marcel Kaheza, Shaaban Stambuli, Yahaya Mbegu, Datus Peter, Mohammed Bakari, Mohammed Yusuph, Kassim Haruna na Christopher John.
https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5


Pole Gerald Mathias Mdamu. Mungu akujaalie upone na kusimama tena.


Wengine ni madereva George Mketo na Vicente Ngonyani na wachezaji wote wapo KCMC wakiendelea na uchunguzi wa daktari, chanzo cha ajali kinachunguzwa.
Polisi imekutwa na janga hilo ikiwa katika maandalizi ya mechi zake za mwishoni za Ligi Kuu inayoelekea ukingoni.