SHABIKI kijana mdogo wa Ureno amewaaga kwa hisia kali mashujaa wake wa timu ya taifa na Cristiano Ronaldo walipokuwa wakienda kupanda ndege kwenda Urusi kwenye fainali za Kombe la Dunia leo.
Ronaldo alikuwa anawaongoza mabingwa hao wa Ulaya kuingia Uwanja wa Ndege wa Humberto Delgado Airport katika mji mkuu wa Ureno, Lisbon ndipo akaitwa na shabiki huyo mdogo aliyekuwa amevaa jezi yenye jina la mchezaji huyo. 
Shabiki kijana mdogo wa Ureno akiagana na Cristiano Ronaldo kwa hisia leo wakati wanakwenda Urusi kwenye fainali za Kombe la Dunia   

RATIBA YA URENO KUNDI B KOMBE LA DUNIA URUSI

Juni 15: Hispania – Sochi – Saa 1:00 uisku
Juni 20: Morocco – Moscow – Saa 7:00 usiku
Juni 25: Iran – Saransk – Saa 1:00 usiku

Nyota huyo wa Real Madrid akasimama kumsikiliza mtoto huyo, akapiga naye picha na kumuacha analia kwa furaha baada ya kumpa autograph kabla ya kuingia kwenye eneo la kwenda kusubiria ndege. 
Ureno imekwenda Urusi leo ambako wanakwenda kupigania kuongeza Kombe la Dunia katika taji la Euro 2016 walilochukua nchini Ufaransa.
Ureno imepangwa Kundi B katika Fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia pamoja na wapinzani wao wa bara moja, Hispania wa wa nje Morocco kutoka Afrika na Iran ya Asia.
Ronaldo na wenzake wataanza kampeni zao za Kombe la Dunia 2018 kwa kumenyana na Hispania mjini Sochi Juni 15, kabla ya kuvaana na Morocco Juni 20 na kumalizia kwa kukipiga na Iran siku tano baadaye.