Mtoto wa Michael Jackson afunguka kuhusu sakata la baba yake

Mtoto wa kike wa Marehemu Michael Jackson, Paris Jackson  amefunguka kwa mara ya kwanza kupitia ukurasa wake wa twitter kuhusiana na makala ya ‘Leaving Neverland’  ambayo ilionyesha mashuhuda wanaodai kufanyiwa vitendo vya ulawiti na baba yake kupitia kituo cha HBO.

Paris Jackson mwenye umri wa miaka 20 amesema kuwa anaamini kuwa marehemu baba yake yupo huru na hahusiki na tuhuma zinazomkabili pia kupitia ukurasa wake wa twitter amezidi kueleza na kusema kuwa “sijaongea chochote kuhusu hili tukio na jinsi linavyoharibu kazi yangu,

“Mmeyawekea maisha yangu umakini mkubwa kuliko ninavyoyachukulia mwenyewe, tulizaneni” >>>Paris Jackson kupitia ukurasa wake wa twitter.

Inaelezwa kuwa tayari vituo vya radio nchini Canada na New Zealand vimeacha kupiga nyimbo za mfalme wa Pop Marehemu Michael Jackson kutokana na wasikilizaji kupaza sauti juu ya makala hiyo na pia inaelezwa hawajajua itachukua muda gani mpaka kuja kurudisha nyimbo za Mfalme huyo katika vyombo vya habari.