NAMUNGO FC YAENDELEA KUGAWA POINTI KUNDI D KOMBE LA SHIRIKISHO, NA LEO IMECHAPWA 1-0 NA NKANA FC NDOLA

TIMU ya Namungo FC imeendelea kugawa pointi katika mechi za Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika baada ya leo pia kuchapwa 1-0 na wenyeji, Nkana FC Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola, Zambia.
Bao pekee la Nkana FC leo limefungwa na kiungo Freddy Tshimenga dakika ya 71 akimalizia pasi yaHarrison Musonda Chisala.
Nkana FC imefikisha pointi sita, kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam Aprili 4 dhidi ya timu hiyo ya Tanzania ikitoka kuchapwa 3-0 na Pyramids nchini Misri na 2-0 na Raja Athletic hapo hapo Ndola.
Namungo FC inaendelea kushika mkia baada ya kupoteza mechi zote nne za awali, ikiwemo kuchapwa 1-0 na Raja Athletic nchini Morocco na 2-0 na Pyramids Dar ed Salaam.
Mechi nyingine ya kundi hilo itafuatia Saa 4:00 baina ya wenyeji, Pyramids na Raja.
Raja ndio inaongoza kundi kwa sasa baada ya kukusanya pointi tisa kufuatia kuzifunga zote, Namungo, Nkana na Pyramids 2-0 Jijini Casablanca. Pyramids ina pointi sita katika nafasi ya pili.

Previous Entries ZAIDI YA VIJANA 48,000 WANUFAIKA NA KAMPENI YA KIJANA NI USAFI. Next Entries PROF MKUMBO AAGIZA UIMARISHWAJI WA SEKTA YA VIWANDA NA BIASHARA ILI ICHANGIE KIWANGO KIKUBWA CHA UKUAJI WA UCHUMI