https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limetoa kibali kwa Mabingwa wa Soka nchini, Simba SC kuingiza mashabiki 10000 katika mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya AS Vita ya DR Congo utakaopigwa Jumamosi ya April 3.

Awali CAF ilizuia Simba kuingiza mashabiki katika mechi zao za nyumbani kwa kisingizio cha hofu ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona hali iliyosababisha Simba icheze bila mashabiki kwenye mchezo wake uliopita dhidi ya El Merreikh ya Sudan ambapo Simba ilishinda kwa magoli 3-0.

Mchezo wa Jumamosi dhidi ya AS Vita ni muhimu kwa Simba kuweza kupata matokeo ya ushindi ama sare ili waweze kufuzu kwa hatua ya robo fainali. Kwa sasa Simba inaongoza kundi lao ikiwa na alama 10 ikifuatiwa na Al Ahly yenye alama saba huku AS Vita wenyewe wakiwa na alama nne na Merreikh wakiwa na alama moja.