Wakati kukiwa na taarifa za mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil anayecheza katika club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar kujutia uamuzi wake wa kujiunga na PSG na kuondoka FC Barcelona, Neymar anahusishwa kutaka kurudi kucheza soka Hispania.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Neymar ambaye leo imethibitika kuwa ataukosa mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Man United kwa kuwa na mejeraha, anatazamiwa kutaka kurudi Hispania huku timu mbili ndio zikipewa nafasi zaidi, Barcelona wanapewa nafasi kama watakuwa wapo radhi kutoa kiasi kikubwa cha pesa.

Real Madrid wao inaaminika wanaweza kufanya kitu kutokana na kuhitaji kuwa na staa mmoja atakayerithi ustaa wa Ronaldo katika uwanja wa Santiago Bernabeu, Neymar anauguza jeraha lake la mguu wa kulia alilolipata katika mchezo dhidi ya Strasbourg, hata hivyo Neymar anadai hana furaha ndani ya PSG na anajutia uamuzi wake ambao alishawishiwa na pesa.