Katika hali isiyo ya kawaida Afisa Habari wa Klabu ya Simba SC Haji Manara ameonekana kama kubanwa na maswali kutoka kwa Waandishi wa Habari wakati wa Mkutano na Waandishi kuelekea Kariakoo Derby.

Moja kati ya swali aliloulizwa Haji Manara ni kuwa takwimu za mechi yao na Yanga SC misimu miwili ya Ligi Kuu hivi karibuni zinaonesha sio nzuri sana kwa Simba licha ya ubora huo waliyokuwanao.

”Kwenye mechi tatu zilizopita, ambazo mmekutana na Yanga kwenye Ligi Kuu hakuna mchezo wowote mliyopata matokeo ya ushindi zaidi ya Mchezo mmoja kufungwa na miwili kutoa sare, ukiizungumzia unazungumzia ni timu kubwa lakini kwa hizi derby kama tatu zilizopita tumeona kwamba Yanga wamekuwa na matokeo mazuri zaidi.”- ameuliza Mwandishi akihoji ubora wa Simba kwenye derby ya mtani hasa akitolea mfano matokeo ya mechi mbili za ligi msimu uliyopita na mchezo mmoja wa msimu huu akijumuisha kuwa wamekutana mara tatu lakini Simba SC imekosa matokeo mazuri licha ya ubora huo wanaousema.

The post Nilikuwa nakusaka, unakuja kuleta uyanga hapa -Haji Manara (+Video) appeared first on Bongo5.com.