Shirika la misaada la Oxfam limesema idadi ya watu wanaokufa kutokana na njaa inavuka ile ya watu wanaokufa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona. 
Shirika hilo limesema idadi hiyo iliongezeka mara sita mwaka uliopita. 
Asasi hiyo ya misaada imebainisha katika ripoti yake kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani kote imeongezeka kuanzia mwaka uliopita kutoka watu wapatao milioni 20 hadi watu milioni 155 na kwamba watu 11 wanakufa kutokana na njaa kila dakika na hivyo kuvuka idadi ya watu wanaokufa kutokana na Covid-19. 
Shirika la Oxfam limesema licha ya hali hiyo, bajeti za kijeshi duniani ziliongezeka na kufikia dola bilioni 51 mwaka uliopita. Imezitaja Afghanistan, Ethiopia, Sudan Kusini, Syria na Yemern kuwa ni nchi zilizo kwenye hali mbaya kutokana na kwamba nchi hizo zimo kwenye mizozo.