PLUIJM ATAKA KUWAMALIZA SIMBA NA YANGA


Kocha mkuu wa timu ya Azam FC, Hans van Der Pluijm, amesema kuwa mipango yake kwa sasa ni kuhakikisha kwamba wanafanikiwa kushinda mechi zote za ligi kuu ili kuweza kuibuka na ubingwa.

Azam wamefanikiwa kushinda mchezo wa pili katika uwanja wa nyumbani Chamazi ambao mchezo wa kwanza walicheza dhidi ya Mbeya City na kushinda kwa mabao 2-0 na mchezo wa pili ni dhidi ya Ndanda walishin­da mabao 3-0.

Kwa mujibu wa Cham­pioni Jumatano, Pluijm alisema kuwa anashangazwa na uwezo wa wachezaji wake wakiwa uwanjani jambo ambalo ana imani kwamba litakuwa na matokeo mazuri katika michezo yao ya ligi kuu.

“Malengo yetu ni kuhak­ikisha kwamba tunafanikiwa kushinda mechi zote ambazo tutacheza nyumbani na ugenini ili kujiweka katika mazin­gira mazuri ya kuweza kuibuka na ushindi kwa kuwa hakuna mwalimu ambaye anafikiria kufun­gwa.

“Nidhamu kwa wache­zaji na ushirikiano ni kitu muhimu ambacho kinatupa nafasi ya kushinda kwa kuwa ushindani kwa sasa ni mkubwa baada ya timu kuongezeka ila hilo halitupi tabu kwa kuwa huwa ninaongea na wachezaji namna itakayo­saidia kuweza kupata matokeo mazuri,” alisema Pluijm.Azam wame­fanikiwa kushinda michezo yao yote miwili dhidi ya Ndanda na Mbeya City ambayo yote im­epigwa Dimba la Chamazi.

Previous Entries Mwalimu Anayedaiwa Kuua Mwanafunzi kwa Kipigo Atiwa Mbaroni Next Entries Inasikitisha! Walezi wa Mtoto wa Darasa la 5 Aliefariki kwa Kipigo cha Mwalimu Waongea kwa Uchungu '‘Hajawahi Kuiba’'