https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5
Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

RAIS Dk.John Magufuli ameagiza flyover ya Mfugale iliyopo makutano ya Tazara ifungwe kamera haraka ili watakaosababisha ajali wawe wanajulikana huku akisisitiza umuhimu wa daraja hilo kutunzwa na isiwe chanzo cha ajali.

Ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anazindua rasmi flyover ya Mfugale ambapo pamoja na mambo mengine amesema ni lazima kamera zifungwe tena haraka.

Rais Magufuli amefafanua “Nataka hapa katika flyover ya Mfugale pafungwe kamera.Tangazenu zabuni haraka kama mtaamua kumpa aliyejenga daraja sawa kama kumpa zawadi.” Daraja hili ni la Mfugale na bahati nzuri Mhandisi Mfugale yupo ,hivyo naamini mtalifanyia kazi haraka,”amesema Rais Magufuli.

Amefafanua kwamba kukiwa na kamera itakuwa rahisi hata ambaye amelewa na akasababisha ajali na kukimbia iwe rahisi kumfahamu na ajulikane.Pia amesema madaraja mengine makubwa na flyover ambazo zitajengwa lazima kufungwe kamera na hiyo itasaidia kulinda miundombinu mbalimbali ya madaraja na flyover.

Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa watanzania kulinda miuondombinu hiyo na kubwa zaidi kuhakikisha haiwi sehemu ya kusababisha ajali na kupoteza maisha ya Watanzania.Wakati huo huo Rais Magufuli amewahakikishia wananchi wa Dar es Salaam kwamba kuna mikakati mingi inaendelea ya kuhakikisha adha ya msongamano wa magar inapungua.

Amezungumzia ujenzi wa flyover mataa ya Chang’ombe pamoja na eneo la Magereza ambapo amesema mazungumzo yalikwishaanza.Pia amesema kuna ujenzi unaendelea eneo la mataa ya Ubungo jumla ya sh.Bilioni 247 zitatumika kwa ajili ya eneo hilo ambapo  katika eneo hilo kutakuwa na daraja la ghorofa tatu,hivyo magari yatakuwa yanapishana juu kwa juu.

Pia amesema tayari ujenzi wa barabara ya mwendo kasi kutoka Mbagala hadi Grezani mchakato wake unakwenda vizuri na itaanza kujengwa.Amesema anataka kuipendeza Jiji la Dar es Salaam na kwamba mipango na mikakati inakwenda vizuri huku akiwahakikishia wananchi wa Jiji hilo kwamba atafanya ziara.