Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla ametoa onyo kwa Wafanyabiashara wanaoendelea kufanya Biashara pembezoni mwa Barabara ya Airport licha ya vibanda vyao kuondolewa kuhama mara moja na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa.

RC Makalla ametoa onyo hilo mapema leo alipotembea mguu kwa mguu kutoka Airport Hadi Chang’ombe kuona utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ambapo ameshuhudia baadha ya Wafanyabiashara wakijiiba na kupika vyakula chini ya miti na kuwataka waondoke na kwenda kwenye maeneo yaliyotengwa.

Aidha RC Makalla amesema kuvunja kibanda na kuendelea kupika Chini ni kazi bure hivyo amewaelekeza
Wakurugenzi,Watendaji wa Kata na Mitaa kuhakikisha wanasimamia Wafanyabiashara hao wasirudi upya.

Hata hivyo RC Makalla amesema kwa unyeti wa Barabara ya Airport atahakikisha anasimamia Barabara hiyo iwe na mandhari nzuri.

The post RC Makalla atoa onyo kali kwa Wafanyabiashara wadogo Machinga (+ Video)

appeared first on Bongo5.com.
https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5