RC Pwani ahaha kumalizia chanjo za corona

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Mkuu wa mkoa wa Pwani Aboubakar Kunenge, amesema kuwa umebaki mwezi mmoja tu kufikia tarehe ya mwisho ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 iliyotolewa ndani ya mkoa huo na kwamba wameanzisha mpango shirikishi utakaowasaidia wananchi kupata chanjo kwa hiari yao popote walipo.
Kauli hiyo ameitoa hii leo Septemba 25, 2021, na kusema kuwa mkoa huo ulipokea jumla ya dozi za chanjo 30,000 lakini hadi sasa ni dozi 15,000 tu ndiyo zilizotumika na hivyo ipo haja ya kutumia mbinu shirikishi ili wananchi wachanjwe kabla ya tarehe ya mwisho ya matumizi ya chanjo haijafika.
“Chanjo 15,000 zilizobaki zimebakisha mwezi mmoja ziharibike na hazitatumika tena baada ya muda huo, hivyo wananchi wenye utayari wajitokeze na kuokoa chanjo iliyobaki kuokoa maisha yao na chanjo isiharibike” amesema RC Kunenge.
Previous Entries VIDEO Rosa Ree – Watatubu Next Entries Download | Rosa Ree – Watatubu | Audio

Leave a Reply

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.