Rich Mavoko aliza watu mtandaoni kwa ujumbe mzito, adai mwisho wa maisha yake umefika

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Rich Mavoko ameacha ujumbe mzito kwenye mitandao ya kijamii ulizua gumzo usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2019.

Rich Mavoko

Rich Mavoko kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika kwa ufupi, akidai kuwa leo ndio mwisho wa maisha yake hapa duniani.

Ni Siku Ya Mwisho Ya Maisha Yangu Yaliobaki” ameandika Rich Mavoko na kuambatanisha picha akiwa mwenye pozi la huruma.

Baadhi ya posti hiyo, wadau mbali walianza kuhoji ni nini? kimejili au kumkuta hadi aweke ujumbe huo huku wengine wakimdhihaki.

teresiamassawe-Wewe mavoko ni kiki unatafuta siyo? Nakuliza?Usimbipu mungu atakupigia.We kama unataka kuachia ngoma mpya lazima urushe vitu vya ajabu mtandaoni? Tena kibaya zaidi eti unasema kifo? Kama ni uwongo utakiona cha moto we haya.

selemanzubery28-duh!!!!! unaniliza bro sana maana na kukubali ile mbaya mwanangu please please usifanye hivyo

luchax_tz-Kunani tena ama ni ile hatrick ya ronaldo ndo inakupa stress c’mon bongo flavor’s Messi😂😂

teresiamassawe-We mavoko acha kiki za ajabu sawa kkngu?Kuna tatizo kweli mlezi wa wasanii yupo MKUU WA MKOA WA DAR PAULO PAKONDA. Nenda atakushauri vizuri

badman_weezy_da_7_eleven-hakuna mtu aijuwae siku yake ya mwishoo brow ni menyezimungu pekee ndo ajuaye 👀. (BE PATIECE BILONEAR KID)

kwetu_pazuri_6-👏ukijitambua mapema akuna shida bro sema nini tusiwatafutie watu kiki kama unakufa kesho leo Anza na safari ya mor mi utanikuta mikese bro tukamarizie ngambe la mwisho.

Kwa taarifa za ndani za watu wa karibu na Rich Mavoko, wamesema kuwa mkali huyo yupo mbioni kuachia wimbo mpya, ambao wamedai utakuwa ni Inspiration Song.

Hata hivyo, Bongo5 imejitahidi kumtafuta Rich Mavoko azungumzie lengo hasa la ujumbe wake, lakini hakuweza kupatikana hewani.

The post Rich Mavoko aliza watu mtandaoni kwa ujumbe mzito, adai mwisho wa maisha yake umefika appeared first on Bongo5.com.

Previous Entries Zonal Developmental Evaluator Job at Social Solutions International, Inc Next Entries 13 Strategy Evaluation Consultancy Jobs at Restless Development Tanzania