BEKI wa Chelsea, Antonio Rudiger, amewashika pabaya mabosi wa klabu hiyo baada ya kuwaambia wampe Pauni 200,000 (zaidi ya Sh mil. 640 za Tanzania) kwa wiki kama wanataka asaini mkataba mpya.

Mkataba wake utafikia ukomo Juni, mwakani, na kwa sasa Mjerumani huyo anapokea Pauni 135,000 (zaidi ya Sh mil. 430).

Wakati Rudiger akiweka sharti hilo, matajiri wa soka la Ufaransa, PSG, wanasikilizia kuona kama Chelsea watashindwa ili wao wajitose kumchukua.

Itakumbukwa kuwa mchezaji huyo alikuwa sehemu ya wachezaji waliotarajiwa kuondoka Stamford Bridge majira ya kiangazi, wakati huo akihusishwa zaidi na AC Milan.