§  Ni kupitia kampeni ya Nje ya Dimba na Stars, mashabiki kukutana na wachezaji kwenye baa zao

 

Bia ya Serengeti Lager leo imezindua kampeni mpya na ya aina yake itakayowawezesha mashabiki wa timu ya taifa, Taifa Stars kukutana na wachezaji nyota wanaowapenda nje ya uwanjani na kufahamu maisha yao ya nje ya soka.

Kampeni hiyo inayojulikana kama  ‘Nje ya Dimba na Stars’ inalenga kuwapa nafasi mashabiki wa Taifa Stars kukutana na nyota wanaowapenda katika baa zao na pia watapata fursa ya kuwauliza maswali kuhusu maisha yao nje ya soka pamoja kupiga nao picha za ukumbusho. Kampeni hiyo ya nchi nzima itadumu kwa miezi mitatu.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, meneja mwandamizi wa chapa wa SBL Wankyo Marando alisema bai ya Serengeti lager ikiwa kama shabiki mkuu wa Taifa Stars inajivunia kuwaletea mashabiki wa Taifa Stars nyota inaowapenda na kuwapa nafasi kuzungumza nao na hivyo kuwafahamu kwa undani zaidi.

“Shabiki mkuu na mdhamini wa timu yetu ya taifa, Taifa Stars Bia ya Serengeti Lager leo inayofuraha kuzindua kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’ inayolenga kuwakutanisha mashabiki uso-kwa-uso na nyota ambao mara nyingi wamekuwa wakiwaona uwanjani. Hii ni fursa pekee ya mashabiki kujua maisha ya nota wao nje ya uwanjani,” alisema Wankyo.

Wankyo alisema kampeni hiyo ya nchi nzima itahusisha wachezaji wa Taifa Stars ambapo watatembelea mikoa ya Mbeya, Mwanza na Arusha na kukutana na mashabiki wao kupitia matukio kama pati za mwisho wa mwezi ‘Nje ya Dimba na Stars’. Kwenye matukio kama hayo mashabiki wataweza pia kujishindia zawadi mbali mbali na ofa za bei yao pendwa ya Serengeti lager.

“Wachezaji watakuwa kwenye baa mbali mbali na wakati wateja wetu wa bia ya Serengeti Lager wakiendelea kuburudika na bia yao pendwa iliyotengenezwa kwa kimea kwa asilimia 100 na isyoongezwa sukari, watapata nafasi ya kuwauliza maswali, kupiga picha na kupata sahihi zao,” alisema

Wankyo aliwataka mashabiki wa Stars kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya bia ya Serengeti Lager Pamoja na kusikiliza redio kwa ajili ya kujua linin a wapi nyota wa taifa Stars watakuwa.

https://t0gkj99krb24.com/hibssfu8iy?key=1199603a84856e9c90eef355de1b36a5

Meneja chapa wa kampuni ya bia ya Serengeti Wankyo Marando (kushoto) akiwaongoza baadhi ya wachezaji wa Taifa Stars kwenye jukwaa kuu, muda mfupi kabla ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’ inayowapa nafasi mashabiki wa Taifa Stars kukutana na wachezaji nyota wanaowapenda uso kwa uso katika baa zao.

 

Baadhi ya mashabiki wa timu ya taifa, Taifa Stars wakipiga picha na wachezaji nyota wa timu hiyo muda mfupi baada ya uzinduzi wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’ inayowapa nafasi mashabiki wa Taifa Stars kukutana na wachezaji nyota wanaowapenda uso kwa uso katika baa zao.

Mchambuzi wa soka Eddo Kumwembe, akimuuliza swali mchezaji wa Taifa Stars Faisal Salum wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Nje ya Dimba na Stars’ inayowapa nafasi mashabiki wa Taifa Stars kukutana na wachezaji nyota wanaowapenda uso kwa uso katika baa zao.